Imetokea nchini India baada ya mama
mmoja kujifungua mtoto mwenye miguu
minne na mikono minne huku akipokelewa
na wenyeji kwa furaha kubwa na kuitwa
'Mungu Mvulana' ....
Mtoto huyo amepewa jina la 'Mungu
Mvulana' kwa kuwa kuzaliwa na viungo
kama hivyo si jambo la kawaida na
huchukuliwa kama mfano wa Mungu kwa
jamii za kihindu na watu walisafiri kutoka
kona mbalimbali za nchi hiyo kwenda
kumshuhudia mtoto huyo wa maajabu.
Katika mji wa Kaskazini mwa nchi hiyo
watu walijazana nje ya eneo la Hospitali
hiyo wakiwa na hamu ya kutaka kumwona
mtoto ambaye ana maana kubwa kwa jamii
za nchini humo na wenyeji wa huko wana
amini ataleta baraka katika jamii zao.
Mamia ya watu walikua wamejaza nje ya
Hospitali hiyo wakiimba na kusali lakini
hawakuweza kufanikiwa kumwona
kutokana na wingi wao huku Polisi
wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia.
Baadhi ya watu walidiriki kusema ujio wa
mtoto uyo ni dalili za mwisho wa dunia
kutokana na jinsi baadhi ya jamii nchini
humo zinavyoamini.
Watalaam wa mambo ya uzazi walisema
kuzaliwa mtoto huyo akiwa katika hali hiyo
ilikua na dalili ya kuzaliwa watoto mapacha
ambao kitaalam wanaitwa Parasitic twins
lakini haikuwezekana na kudai ni mipango
ya Mungu.
Familia ya mtoto huyo imejawa na furaha
kwa ongezeko la mwanafamilia mwingine
na wanamuona mtoto huyo kama Mungu,
mtoto wa kiume wa familia ya
Wahindu,Brahma ambaye anatambulika
kwa kuwa na miguu na mikono minne.
No comments:
Post a Comment